Monday, 8 June 2015

HIVI UNAZIFAHAMU FAIDA HIZI ZA KABICHI?


Najua wengi tunaifahamu sana kabichi kama mboga na baadhi yetu tunaitumia sana katika maisha yetu ya kila siku.

Lakini leo nimeona ni vyema tufahamishane hizi baadhi ya faida zinazopatikana kupitia kabichi.

Moja ya faida za kabichi ni ule uwezo wake wa kuwasaida wale wenye nia au malengo ya kupunguza miili yao au wanene kupita kaisi. sifa hiyo inatokana na kalori ndogo zilizomo ndani ya kabichi pamoja na ufumwele mwingi.

Aidha, ulaji wa kabichi pia huweza kumsaidia mwili kujenga kinga madhubuti dhidi ya magonjwa hatari ikiwemo saratani. Kabichi imeonekana kuwa na uwezo wa kipekee wa kupambana na ugonjwa huu kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha aina tatu muhimu za mada za 'Antioxidant', 'Anti-inflammatory' na 'Glucosinolates,' ambazo zina uwezo wa kudhibiti magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababisha saratani za aina mbalimbali mwilini.
Hizi ni aina za kabichi
Pamoja na kuwa mboga hii ya kabichi si mboga pendwa sana na watu wengi, lakini ni mboga yenye kiwango cha kutosha cha aina mbalimbali za vitamin hasa vitamini K, B1, B2, vitamin A na C. Pia kabichi ina kiasi kingi cha ufumwele au kamba lishe kwa maana ya fiber, ambapo vyote hivyo ni kinga ya mwili dhidi ya magonjwa nyemelezi.

Hizi ni faida za kabichi nimeona ni vyema uzipate leo kutoka kwetu Mandai Herbalist Clinic, lakini kwa maoni na ushauri zaidi unaweza kuwasiliana na Dk.Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe dkmandaitz@gmail.com Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu

No comments:

Post a Comment