Saturday, 13 June 2015

HOMA YA MATUMBO YASIMAMISHA MASOMO NCHINI ZAMBIA


Shule 30 zimefungwa nchini Zambia katika mji mkuu wa Lusaka baada ya kuzuka kwa homa ya matumbo.

Shule hizo zimeripotiwa kufungwa baada ya mwanafunzi mmoja kufariki kutokana na maradhi ya homa ya matumbo.

Hatua hiyo imefuatiwa na hali ya uchafu wa mazingira.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Jamii katika manispaa ya mji Mulunda Habenzu, aliarifu kufungwa kwa shule hizo zilizokuwa katika eneo la Kanyama, magharibi mwa mji wa Zambia.

Hadi kufikia sasa, mwanafunzi mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 11 amepoteza maisha huku wengine wawili wakipatiwa matibabu.

Nayo Wizara ya Afya ya Zambia imetangaza kuchukua hatua thabiti ili kuzuia maradhi hayo kuenea katika sehemu nyingine za mji huo.

Naibu Waziri wa Afya wa Zambia Chitalu Chilufya, amesema kwamba kesi 36 za maradhi ya homa ya matumbo zimegunduliwa katika eneo la Kanyama na hali ya afya imeweza kudhibitiwa.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment