Friday, 5 June 2015

IDADI YA WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA MOTO NCHINI GHANA YAONGEZEKA


Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa karibu wa vyombo vya habari basi naamini jana Alhamisi utakuwa uliipata ile taarifa ya watu 96 kupoteza maisha kutokana na ajali ya moto iliyotokea katika kituo cha mafuta katika mji mkuu wa Accra nchini Ghana.

Sasa ripoti mpya iliyotoka leo ni kwamba idadi ya vifo imeongezeka ambapo hadi sasa watu waliofariki nchini humo wamefikia 175 kutokana na ajali hiyo.

Lori ambalo lilibeba miili ya watu waliokufa kwenye ajali hiyo lilikuwa likichirizisha damu

Kufuatia vifo hivyo Serikali ya Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa .
Baadhi ya magari yaliyoteketea kwa moto huo
Moto huo ulizuka siku ya Jumatano usiku wakati mvua kubwa ikinyesha ambapo wakazi wa mji huo walikuwa katika eneo hilo wakijikinga na mvua hiyo ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na kukosekana kwa umeme kwa muda mrefu.

 Poleni sana kwa msiba huu mzito ndugu zetu Waghana

No comments:

Post a Comment