Thursday, 11 June 2015

IFAHAMU NCHI YENYE IDADI KUBWA YA WABUNGE WANAWAKE BARANI AFRIKA
Imeelezwa kuwa Rwanda ni moja ya nchi barani Afrika yenye idadi kubwa  ya wabunge wanawake katika bunge la Rwanda.

Ongezeko hilo linafuatiwa na jitihada za wanawake hao za kuwajibika kiuchumi na kijamii ambazo zinaelezwa kuwawezesha wanawake kupata viti 51 kati ya 80 bungeni.

Umoja wa bunge hilo umeeleza katika ripoti kuwa nafasi hiyo waliyoipata wanawake bungeni ni muhimu na ya kipekee duniani kote na kwamba imepita kiwango kilichotarajiwa na Marekani.

Mmoja wa wabunge wadogo kabisa, Justine Mukubeya mwenye umri wa miaka 28 amesema "mimi ni mbunge mdogo kuliko wote nchini Rwanda na nafasi hii tuliyoipata inaonyesha hali ya maendeleo nchini Rwanda".

Pia inaelezwa kuwa kwasasa, nafasi nyingi za juu wamepewa wanawake nchini humo, huku majina mawili ya wanawake nchini Rwanda yakiwa yamewekwa katika orodha ya wanawake 50 wenye ushawishi mkubwa duniani orodha iliyoandaliwa na jarida moja nchini Ufaransa.

Rwanda ni moja ya nchi zinazoendelea kwa kasi barani Afrika licha ya kukumbwa na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambayo yalisababisha vifo vya watu wengi na maelfu ya wananchi kuyahama makazi yao.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic  kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment