Wednesday, 24 June 2015

ILE HOJA YA KUHUSU TOZO ZA MAFUTA YA TAA BUNGENI IKASABABISHA WAZIRI KUJA NA HAYA MAJIBU YA KIUTAFITI ZAIDI!!


Mafuta ya taa ni moja ya bidhaa ambayo imekuwa ikitumiwa na watu wengi hapa nchini hususani wale waishio maeneo ya vijijini.

Hivi karibuni katika bunge la bajeti serikali kupitia Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ilipendekeza mafuta hayo ya taa kuwekewa tozo ya kiasi cha shilingi 100 kama ilivyo katika mafuta ya petroli na diseli, huku lengo likiwa ni kuweka ulinganifu ili kila mtanzania achangie japo kidogo.
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum

Kufuatia hoja hiyo  baadhi ya wabunge wamekuwa wakilalamika kwamba kuwatoza wananchi Shilingi 100 katika mafuta ni kuwanyanyasa. Jambo ambalo limekuwa likikanushwa na serikali


Pata nafasi ya kumsikia hapa Waziri wa Fedha Saada Mkuya akieleza juu ya hili. Karibu usikilize...

No comments:

Post a Comment