Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 17 June 2015

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA PALE INSPEKTA JENERALI WA POLISI (IGP) OMARY MAHITA ALIPOTEMBELEA MANDAI HERBALIST CLINIC (PICHA)Aliyewahi kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali IGP Omari Mahita ambaye alistafu mwaka 2006 leo Juni 17, 2015 ameaua kutembelea Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Katika matembezi yake hayo IGP mstaafu aliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic, Tabibu Abdallah Mandai ambapo IGP Mahita alionekana kufurahishwa na huduma zitolewazo kituoni hapo pamoja na uwepo wa vifaa vya kisasa na madhari mazuri ya kituo.

Hapa ninazo picha za Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita alipokuwa akitembezwa ndani ya kituo cha Mandai Herbalist Clinic kwa lengo la kujionea huduma mbalimbali zitolewazo na kituo hiki. Karibu utazame picha.......

Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita akiwa ndani ya chumba kinachotumika kwaajili ya wagonjwa kufanyiwa massage akipewa maelekezo kutoka kwa Dk. Abdallah Mandai ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic.

Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita akipokea maelekezo kutoka kwa Dk. Mandai kuhusu mashine inayoonekana hapo nyuma jinsi inavyofanya kazi
 
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita akiwa amepanda kwenye moja ya mashine yenye uwezo wa kupunguza vitambi na kuimarisha joint na mzunguko wa damu mwilini (kulia) ni mtaalam wa mifupa Mathayo Masinema kutoka Mandai Herbalist Clinic


Dk. Mandai (kulia) akimuonesha Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita moja ya mashine inayotumika kwaajili ya  kuchua kwa wale wenye maumivu ya viungo na waliopooza pia.
Dk. Mandai (kulia) akimuonesha Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita mfano wa namna mashine hiyo ya kuchua (massage) inavyofanya kazi.
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita (kulia) akifurahi jambo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa Dk. Mandai walipokuwa ndani ya chumba cha dawa
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita (kulia) akiwa na Dk. Mandai (kushoto)ndani ya chumba cha kitengo cha habari cha Mandai Herbalist Clinic
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita (kulia) akisalimiana na Dk Msaidizi Mudy Mandai  mara baada ya kufanyika kwa utambulisho kutoka kwa Dk. Abdallah Mandai
Dk. Abdallah Mandai (katikati) akimuelezea Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita namna kazi zinavyofanyika kituoni hapo
Hapa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita (kushoto) akisalimiana na Mzee Omary Athumani kutoka Zanzibar mwenye miaka 87 ambaye wanafahamiana na walijikuta wakionana hapo kituoni
Kati ya mambo aliyozungumza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita alipokuwa Mandai Herbalist Clinic ni pamoja na kuainisha kwamba yeye ni mmoja wa watu wanaoamini sana tiba asili na kikubwa anaamini kuwa hata hizo tiba za kisasa zilianza kuwa tiba asili kwanza.


Mandai Herbalist Clinic ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dk. Abdallah Mandai tunapenda kutoa shukrani zetu nyingi kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) mstaafu Omari Mahita kwa kuamua kutembelea kituo chetu na kuridhika na huduma tunazozozitoa pia, hii ni kiashiria tosha kwamba hata viongozi wakubwa wanazitambua tiba asili.

No comments:

Post a Comment