Wednesday, 24 June 2015

ISHU YA TOZO ZA MAFUTA YA TAA NI MOJA YA MAMBO AMBAYO YALIYOZUNGUMZWA JANA BUNGENI MJINI DODOMA, FAHAMU WAZIRI WA FEDHA ALICHOSEMA KUHUSU HILO


Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
BUNGE jana lilifanikiwa kupitisha bajeti ya Serikali ya Shilingi trilioni 22.5 kwa mwaka ujao wa fedha baada ya asilimia 83 ya wabunge kuipigia kura ya ndiyo.

Miongoni mwa hoja zilizopata nafasi ya kuzungumzwa jana bungeni ni pamoja na hoja za utetezi wa kodi ya mafuta ya taa.

Ambapo katika suala hili Waziri Fedha, Saada Mkuya Salum, alisema ni lazima zilipwe na kila Mtanzania anayeyatumia ili kuiwezesha Serikali kufanikisha mpango wake wa kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA).


Nimeamua kukurekodia msomaji wangu sauti ya Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, wakati alipokuwa akizungumzia suala hilo, hebu chukuwa dakika yako 1 na sekunde 33 kumsikiliza hapa Waziri akizungumzia suala hilo.

No comments:

Post a Comment