Wednesday, 17 June 2015

JE, HUWA UNASUMBULIWA NA TATIZO LA KUVIMBA MIGUU? TUMIA MCHAI CHAI KUJITIBU


Mchai chai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake.

Wengi tumekuwa tukiutambua mmea huu kama kiungo katika chai ambacho husaidia sana kuleta harufu nzuri zaidi katika chai.

Tumekuwa tukipokea maswali mengi kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza kuhusu mmea huu ikiwa unaweza kutibu tatizo lolote. Maswali mengi tumekuwa tukiyapata kupitia ukurasa wetu wa facebook uitwao Mandai Herbalist Clinic- mhc.

Moja ya kati ya matatizo ambayo huweza kupatiwa suluhisho kwa kutumia mchai chai ni pamoja na tatizola kuvimba miguu.

Unachopaswa kufanya endapo unatatizo hilo ni kutafuta majani ya mchai chai kisha yachemshe na uchuje halafu kunywa maji hayo kila siku jitahidi kwa siku umalize lita moja na utaona mabadiliko.

Pia mmea huo husaidia kukabiliana na tatizo la baridi yabisi, kusafisha figo, kuwasaidia wale wenye shida ya matumbo kuunguruma na hivyo kumsaidia mhusika kurejea katika hali ya kawaida.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.  

 No comments:

Post a Comment