Thursday, 25 June 2015

JE, ILE SAFARI YA KISIASA YA WEMA SEPETU ITAMFANYA MWANADADA HUYO KUACHANA NA SANAA? NA VIPI KUHUSU YALE MAVAZI YAKE NAYO?


Jana June 24 msanii wa bongo movie mwanadada Wema Sepetu alipata nafasi ya kuonekana kupitia Clouds Tv ndani ya kipindi cha Clouds 360 na katika mambo ambayo aliyazungumza ni pamoja na ile safari yake ya kisiasa aliyoianza ili kuelekea bungeni.

Wema katika mahojiano yake hayo alisema kuwa amezaliwa kwenye familia ya siasa kwani  marehemu baba yake alikuwa mwanasiasa, huku akisema kuwa mzazi wake huyo wa kiume aliwahi kumwambia kuwa angependa aingie kwenye siasa

"Marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kwamba anatamani niingie kwenye siasa, mwaka 2010 nilikuwa siko tayari.. nimejisikia vibaya baba yangu amefariki wakati sijaonesha kwamba ninaweza kufanya, nina uhakika kule aliko anajisikia fahari. "

Aidha, Wema alipoulizwa ni kwanini amaeamua kugombea Singida na si kwingineko alisma kuwa “Mama yangu ametoka Singida, nimeona hiyo ndio sehemu nzuri ya kwenda kugombea na huu ndio muda sahihi… nadhani ninaweza kujitolea kwa jamii yangu kwa sababu Singida ni nyumbani“
Akiainisha kuhusu kipaumbele chake endapo pale atapata nafasi hiyo ya ubunge Wema alisema kuwa “Kipaumbele changu kitakuwa ni wanawake, kwa sauti yangu na ushawishi wangu ninajua kwamba nitaweza”

Pamoja na hayo msanii huyo amesema ikiwa atapata nafasi hiyo ya ubunge hawezi kuacha usanii

"Siwezi kuacha sanaa kwa sababu ya Ubunge, nilikuwa na shughuli zangu kabla ya Ubunge, siwezi kusema ninaacha kabisa kila kitu kwa sababu ya Ubunge"


Hata hivyo kumekuwa na picha mbalimbali katika mitandao ya kijamii zikimuonesha mwanadada huyo akiwa ameanza kubadili namna ya mitindo ya kimavazi na sasa ameanza kujiweka kisiasa zaidi.

Cheki hapa chini picha zake za sasa

 
 
No comments:

Post a Comment