Wednesday, 17 June 2015

JE, ULIPITWA NA HII STORY YA MWIGIZAJI WEMA NAYE KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE? IPO HAPA


Muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu jana Juni 16, kupitia kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM amesema kuhusu uamuzi wake wa kuchukua fomu ya ubunge wa viti maalumu mkoani Singida

Akizungumza na mtangazaji Diva Loveness wa Ala za Roho alisema..”Sasa hivi niko Singida kwenye maandalizi ya kuchukua fomu kwasababu nagombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa singida, kwa hiyo nimekuja huku kuja katika kuhamasisha vijana wajitokeze kujiandikisha kwenye daftari la kupigia kura, nimekuja kujiandikisha huku kwa sababu mama yangu ni mtu wa Singida so nimejiandikisha tayari tukutane 15 tena kuja kuchukua fomu"

Aidha, aliongeza "inshallah tuombe uzima, kampeni zimeshaanza zile ndogo ndogo nashukuru Mungu naendelea vizuri nahitaji support kwa jamii "


Pamoja na hayo, mrembo huyo amesema kuwa "watanzania wajue tu yes nitachukua fomu ya kugombea Ubunge wa viti maalumu ya mkoani Singida and tutaona uko mbele itakavyokuwa kwasababu hiki ni kinyang’anyiro naingia katika ni kama vile naingia kwenye mapambano yaani vitaani so kuna kupata na kukosa lakini si fikiri kukosa kwasababu mtu ukifikiri kukosa unajiweka kwenye negative side sana lakini najua kwa nguvu za watanzania na kwa nguvu za wananchi wa Singida wataweza kuniamini na kunipa kura zao."


Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu. 


No comments:

Post a Comment