Thursday, 4 June 2015

JE, UMEKOSA RAHA KUTOKANA NA TATIZO LA FANGASI SEHEMU ZA SIRI? JIBU LAKO LIPO HAPA


Baadhi ya wanawake wamekuwa wakikosa raha ya maisha kutokana na kusumbuliwa na fangasi wa sehemu za siri (ukeni) ambazo husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans.

Ugonjwa huu ni kati ya magonjwa ambayo huwasumbua wanawake mara kwa mara.

Miongoni mwa njia ambazo huchangia kuambukiza kwa ugonjwa huu ni pamoja na matumizi ya vyoo vichafu na kuchangia nguo za ndani pia.

Mbali na hayo joto pamoja na unyevu mwingi na nguo za kubana pia huweza kuchangia kutokea kwa fangasi hizi za sehemu za siri (ukeni)

Mbaya zaidi ugonjwa huu huweza kuambukizwa kwa njia ya ngono endapo mhusika mwenye tatizo hili atakutana kimwili na mwenza wake ambaye hana maambukizi bila kutumia kinga.

Fangasi huweza kuwa na dalili zifuatazo:

Kuwashwa sehemu za siri hasa kwenye uke na sehemu za mashavu ya uke.

Kutokwa na maji maji meupe mfano wa maziwa kutoka kwenye uke ambayo wakati mwingine huweza kuwa na harufu.

Kupatwa na maumivu wakati wa kukojoa kwa baadhi ya wagonjwa.

Ili kuepuka kupata ugonjwa huu inashauriwa kuvaa nguo za ndani zilizokauka vizuri na kuzingatia usafi wa sehemu za siri na kujikausha vizuri mara baada ya kuoga pamoja na kuimarisha usafi wa choo.

Pamoja na kukueleza yote hayo kuhusu tatizo hili la fangasi sehemu za siri, lakini habari njema ni kwamba Mandai Herbalist Clinic tuna dawa nzuri sana kwa ajili ya kumaliza kabisa tatizo hilo tena kwa haraka kama ungependa kuipata wasiliana nasi sasa kwa namba za simu zifuatazo: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment