Thursday, 4 June 2015

JE, UNGEPENDA KUPUNGUZA UZITO WAKO LEO?Suala la uzito mkubwa ni moja ya mambo ambayo yamekuwa kikwazo kwa  baadhi ya watu miaka ya hivi karibuni hususani kinadada.

Hapa kuna hizi njia ambazo zitaweza kukusaidia kupunguza uzito wa mwili wako.

Acha au punguza kula vyakula vilivyopikwa na mafuta mengi. Unapokula sana vyakula hivyo hupelekea kuongeza mafuta mwilini na kukusababisha unene ambao sio mzuri kwa afya yako.


Punguza kutumia vyakula vya wanga (mchele, mikate, tambi n.k) badala yake penda kula mboga mboga za majani na matunda kwa wingi, lakini pia kuhusu vinywaji unaweza kunywa juisi ya malimao ambayo husaidia kuyeyusha mafuta tumboni.


Juisi ya malimao
Penda kuwa mnywaji wa maji mara kwa mara angalau hata kiasi cha lita mbili kwa siku.

Jambo lingine la msingi ni kufanya mazoezi mara kwa mara angalau kwa dakika 30 kila siku. Hivyo unaweza kufanya mazoezi ya kukimbia au kuendesha baiskeli kwa kilometre chache au jaribu kutembea kwa angalau dakika 45 kwa siku.

Kimsingi mazoezi yatasaida mwili wako kuwa mwepesi ni vizuri kufanya mazoezi hadi pale unapotokwa na jasho kwasababu kutokwa na jasho ni kipimo cha kuwa umefanya mazoezi kwa kiwango kinachotakiwa lakini jambo zuri zaidi kutokwa na jasho ni namna ya asili ya kuondoa sumu na uchafu mwilini.

Pata muda wa kupumzika vya kutosha ili mwili upate muda wa kutumia chakula cha ziada kilichopo mwilini wakati wewe unapokuwa umepumzika.

Pia unapofika kwetu Mandai Herbalist Clinic tutakusaidia kupata suluhisho la tatizo hilo la kuwa na uzito mkubwa. fanya jitihada za kuwasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment