Thursday, 11 June 2015

JUISI YA NYANYA INAUWEZO WA KUREFUSHA KIPINDI CHA UZAZI KWA WANAWAKE


Ni mara kadhaa tumekuwa tukizungumzia kuhusu umuhimu wa nyanya na juisi yake katika miili yetu sasa leo kuna huu utafiti uliofanyika huko nchini Tokyo kuhusu juisi ya nyanya

Kwa mujibu wa utafiti huo ulifanywa na Chuo Kikuu cha Udaktari cha Tokyo, Juisi ya nyanya imekuwa jibu kwa wanawake wengi duniani katika ile ndoto yao kubwa ya kupunguza madhara ya kufikia kikomo cha kuweza kubeba ujauzito yaani ‘menopause’.

Kufuatiamajibu ya utafiti huo wataalamu kutoka chuo hicho wametoa ushauri kwa wanawake kunywa vikombe viwili vya juisi ya nyanya kwa siku kwa ajili ya kutatua matatizo hayo.

Aidha, nao wanasayansi wa Japani wao wamesisitiza kunywa mara mbili kwa siku juisi hiyo ambayo ni sawa na mililita 200 ya juisi hiyo ya nyanya kwa muda wa wiki 8.

Mbali na hayo, pia inasadikika kuwa juisi ya nyanya inauwezo wa kupunguza matatizo mengi yakiwemo msongo wa mawazo, homa kali na hali ya kukasirika.

Pia wanasayansi hao walisisitiza kuwa juisi ya nyanya hupunguza mafuta kwa kasi zaidi, hivyo itakuwa faida kubwa kwa wanawake wengi duniani.

Unaweza kuwasilina na Dk. Mandai kama unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo yale sugu. Unachopaswa kufanya ni kupiga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.


No comments:

Post a Comment