Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Monday, 29 June 2015

KAMA ULIKUWA HAUJUI UMUHIMU WA CHOROKO BASI KUANZIA SASA TAMBUA KUWA ZINA MANUFAA SANA KATIKA AFYA YAKO


Choroko ni moja ya mboga ambayo mara nyingi huonekana kama imesaulika sana na kukosa wapenzi au washabiki wengi ndani ya familia zetu nyingi.

Mboga hii huenda imeonekana kukosa mashabiki pengine kutokana na wengi kutoijulia namna sahihi na nzuri ya kuipika, lakini leo sina lengo la kwenda huko kwenye maishi ila ipo siku nitakupa namna nzuri ya kuipika mboga hii.

Jambo la msingi ni kwamba ikiwa wewe ni mtumiaji mzuri wa choroko basi utakuwa unanufaika na virutubisho muhimu vinavyotokana na mboga hii.

Mboga hii ya choroko ni moja ya chakula chenye kiwango kikubwa cha protini, madini ya 'phosphorus' pamoja na yale ya kalsium.


Miongoni mwa faida anazopata mlaji wa choroko ni pamoja na kuimarisha mifupa, hii ni kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya 'phosphorus' na kalsium.

Pamoja na hayo, choroko pia ni nzuri kwa afya ya moyo kutokana na mafuta yaliyopo kwenye mboga hii kuwa salama kwa afya ya moyo na kuufanya moyo kufanya kazi zake vizuri zaidi.
  
Ndugu yangu kama unateseka na magonjwa mbalimbali ni vyema ufanye utaratibu wa kuwahi kufika Mandai Herbalist Clinic sasa ili upate suluhisho la matatizo yako ya kiafya. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment