Wednesday, 17 June 2015

KITUNGUU MAJI NI KIUNGO AMBACHO KIKITUMIKA VIZURI HUWA NI DAWA


Kitunguu maji ni moja ya kiungo ambacho hutumiwa sana katika kukamirisha mapishi mengi jikoni, lakini kiungo hiki pia ni tiba kwa matatizo ya afya zetu.

Kitunguu maji kinauwezo mkubwa wa kuwasaida wale wenye shida ya haja ndogo (mkojo) kuuma.

Ili kutatua tatizo hilo inapaswa kuponda kiasi cha gramu sita ya vitunguu na baadaye kuchemsha katika nusu lita ya maji na kuiacha ichemke hadi pale itakapo pungua nusu ya ule ujazo wote kisha mpatie mgonjwa anywe.

Adha, kitunguu pia kinauwezo wa kutibu tatizo la kikohozi, vidonda vya tumbo, ngozi, figo pamoja na tumbo.

Kwa tatizo la kikohozi kinachotakiwa kufanyika ni kuchukua kitunguu maji kimoja kikubwa na ukikate kate kwenye maji kisha chemsha maji hayo kwa dakika tano na baadaye mgonjwa anywe kijiko kikubwa kimoja kutwa mara tatu yaani asubuhi mchana na jioni.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.  


No comments:

Post a Comment