Saturday, 6 June 2015

KUFUATIA TEMBO KUFA KUTOKANA NA TATIZO LA UJANGILI, SASA IMEBIDI KUANZISHWA KWA KITUO CHA TEMBO YATIMA!Kwa kawaida tumezoea kushuhudia vituo vya kulelea watoto waliopoteza wazazi wao maarufu kama vituo vya watoto yatima, lakini hii ya leo huenda ikawa ni idea mpya kabisa kutoka kwenye sekta ya utalii.

Unaambiwa kuwa Tanzania imeamua kuanzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima kilichopo mjini Arusha.

Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine.

Aidha, kituo hicho kinatarajiwa kutoa uangalizi kwa tembo wadogo wapatao 40, na watahifadhiwa mpaka watakapokuwa wakubwa na hatimae kurudishwa katika mazingira yao halisia.

Hatua hiyo ya serikali ya kuanzisha kituo hicho inakuja baada ya utafiti wa serikali kubaini kuwa Tanzania hupoteza takriban tembo 30 kila siku.

Katika mahojiano ya hivi karibuni na BBC, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amebaini kwamba katika hifadhi ya taifa ya Ruaha pekee, tembo wapatao 12,000 walitoweka katika kipindi cha mwaka mmoja.

Pia Waziri Nyalandu amekiri kwamba kiwango hicho ni kikubwa mno na kwamba kinatia wasiwasi, hivyo kuongeza kwamba uchunguzi umefanyika kubaini chanzo cha tatizo hilo.

Asante mdau wetu kuendelea kuwa nasi katika kupata taarifa mbalimbali kutoka kwetuu, tambua tunathamini sana uwepo wako.

No comments:

Post a Comment