Sunday, 28 June 2015

KUKUTWA UNAKOJOA HADHARANI NCHINI INDIA SI ISHU NDOGO, KUNA ADHABU YAKE NA FAINI PIA


Hapa bongo si ajabu sana kumkuta mtu mzima akiwa na akili zake timamu akitoa haja ndogo (kukojoa) yake hadharani tena kweupe kabisa, lakini nchini India ukikutwa unafanya tukio hio ni kifungo.

Sasa huko nchini India taarifa zinaeleza kuwa Polisi waliwakamata takribani watu 109 wakiwa wanakojoa hadharani katika vituo vya usafiri wa umma na reli.

Watu hao wote inaelezwa wamehukumiwa kifungo cha siku moja jela au kulipa faini ya kati ya dola mbili na kumi au kutumikia vyote kwa pamoja kutokana na kutenda kosa hilo.

Aidha, Maafisa wa Afya ya Umma nchini humo wanasema walifanya operesheni hiyo kwa ghafla ili kukabiliana na uvundo wa mkojo unaoathiri afya za mamilioni ya watu wanaotumia huduma hiyo ya reli nchini India.

Naye, Mkuu wa Polisi katika eneo hilo GRP, Gopeshnath Khanna aliyeongoza operesheni hiyo anasema kuwa operesheni hiyo itakuwa ni endelevu na itawashughulikia pia na wale wanaotema mate ovyo.

Operesheni hiyo ni sehemu ya kampeini ya Waziri Mkuu Mpya wa India, Narendra Modi ambayo imelenga kuimarisha afya ya umma na imepewa jina la kampeni ya 'Swachh Bharat.

Pamoja na hayo, takwimu za afya nchini humo zinaonesha kuwa takriban watu milioni mia sita ama nusu ya raia wa India wanaishi bila kuwa na vyoo.

Kwa stori nyingine nyingi na taarifa mbalimbali, tafadhari endelea kuwa nasi kila siku na utaweza kuyafahamu mengi sana kutoka kwetu, lakini kama unatatizo lolote la kiafya basi unaeza kuwasiliana na Mandai Hebalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment