Saturday, 20 June 2015

KUMBE KUNAWANAUME AMBAO HUKUMBWA NA MATUKIO YA KUBAKWA? KUNA HOSPITALI IMEAMUA KUANZISHA KLINIKI MAALUM KWAAJILI YAO!!!


Story za wanaume kubakwa mara nyingi tumekuwa tukizisikia tu mitaani na ni mara chache sana kuwashuhudia live waathirika wa matukio hayo wakijitokeza kwenye vyombo vya sheria kudai haki zao kutokana na kutendewa vitendo hivyo.

Sasa leo kuna hii stori kutoka mjini Stockholm nchini Sweden ambapo huko kuna hospitali moja ambayo inatarajia kufungua kliniki ya kwanza ya wanaume waliobakwa.

Hospitali hiyo ya South General Hospital tayari ina eneo linalotoa huduma ya dharura kwa wanawake waliobakwa ama kunyanyaswa kijinsia.

Lakini siku ya Jumatano hospitali hiyo ilitangaza kuwa itaanza kuwalaza wavulana na wanaume kuanzia mwezi Octoba.

Taarifa zinasema kuwa ni takriban visa 370 vya unyanyasaji wa kijinsia miongoni mwa wanaume na wavulana viliripotiwa nchini Sweden mwaka uliopita kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

Daktari Lotti Helstrom aliiambia redio ya Sweden kuwa swala la wanaume kubakwa ni miko, lakini limeongezeka kwa kiwango kikubwa bila watu kujua.

Daktari huyo amesema kuwa ni muhimu kwa wanaume kupewa huduma za dharura sawa na wanawake.
  
Shukrani kwa kuendelea kupitia tovuti hii mara kwa mara, tambua tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu, tunaomba uendelee kuwa nasi kila siku kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali

No comments:

Post a Comment