Saturday, 20 June 2015

KUMBE WATOTO WANAODANGANYA HUWA NA KUMBUKUMBU NZURI ZAIDI KULIKO WALE WASIO DANGANYA!!


Kuna ule usemi usemao kuwa ukiwa muongo basi uwe na kumbukumbu. Inawezekana usemi huu ukawa na ukweli ndani yake kutokana na utafiti uliofanyika nchini Uingereza.

Wanasayansi nchini humo wanasema kuwa wana ushahidi kwamba watoto wanaodanganya bila mtu kugundua wana kumbukumbu nzuri ikilinganishwa na wale wasiodanganya.

Watafiti hao kutoka katika Chuo Kikuu cha Sheffield kwa siri walichukua filamu ya watoto wa umri wa miaka sita na saba wakifanya mtihani uliokuwa na majibu ambayo yalikuwa yameandikwa nyuma

Wale waliodanganya kuhusu kile waliochofanya walifanya vyema kutokana na uwezo wao kukumbuka walichofunzwa.

Mmoja ya watafiti hao Elena Hoicka alisema kuwa sababu kuu ni kwamba wale wanaodanganya hulazimika kukumbuka ukweli wote pamoja na uwongo.

Shukrani kwa kuendelea kupitia tovuti hii mara kwa mara, tambua tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu, tunaomba uendelee kuwa nasi kila siku kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali 

No comments:

Post a Comment