Advertisement

Advertisement

Shop

Shop

Mixer

Mixer

Saturday, 27 June 2015

KUTANA HAPA NA MAELEZO YA DK MANDAI KUHUSU MATATIZO YA FIGO


Figo ni miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji kazi wa mwili wa binadamu.

Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa kazi ya kiungo hiki ni kuchuja uchafu ulio kwenye damu na kwa kawaida mwili wa binadamu huwa na figo mbili zenye maumbo yanayofanana ambazo ziko kila upande wa uti wa mgongo, na zimejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo ya mbavu.

Kazi ya figo ni kuchuchuja maji yasiyohitajika mwilini, huku zikinyonya madini na kemikali muhimu na kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje uchafu usiohitajika.

Hivyo figo zina jukumu kubwa katika mwili, sio tu kuchuja uchafu kwenye damu, bali pia na kuratibu madini yaliyomo ndani ya damu, shinikizo la damu na kuchochea uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu.

Dk. Mandai anasema pia figo huchuja uchafu wa vyakula vilivyosharabiwa mwilini na huzalisha homoni ya 'erythropoietin' ambayo huchochea uti wa mgongo kuzalisha chembechembe nyekundu za damu.

Baada ya figo kuchuja uchafu, mkojo huzalishwa na kupelekwa kwenye kibofu kupitia mrija wa ureta ambako huhifadhiwa hapo ukisubiri kutoka nje ya mwili kwa kukojoa.

Miongoni mwa sababu ambazo huchangia figo kushindwa kufanya kazi ni pamoja na shinikizo la juu la damu na ugonjwa wa kisukari.

Daktari anaeleza kuwa pale kunapokuwa na shinikizo kubwa la damu kuliko ukubwa wa mishipa yake husababisha ugonjwa wa moyo na pia ugonjwa sugu wa figo.

Sababu nyingine ni kuharibika kwa seli zinazohusika na uchujaji wa uchafu hali inayosababisha kupungua kwa mkojo, kutotolewa kwa protini katika mkojo na kuvimba kwa mikono na miguu.

Mara nyingi dalili za ugonjwa wa figo huchelewa sana kujitokeza na wakati mwingine mwenye tatizo huwa hahisi dalili yoyote, hadi pale inapotokea akaugua ugonjwa mwingine na daktari kuhisi tatizo, ndipo hugundulika kuwa na ugonjwa huo baada ya vipimo.

Aidha, Dk Mandai anasema kuwa sababu zinazotajwa kupelekea figo kushindwa kufanya kazi ghafla, ni pamoja na kuwepo kwa sumu mwilini, kushuka kwa kiwango cha mzunguko wa damu. Huku sababu nyingine ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa moyo, ambapo moyo hushindwa kusukuma damu kwa ghafla.

Dalili za matatizo haya ya figo ni pamoja na kuongezeka kwa uchafu ndani ya mwili ambao husababisha kwanza kabisa kupungua kwa kiasi cha mkojo, kushindwa kupumua, kusikia kichefuchefu, kutapika na kuvimba miguu.

Dalili nyingine ni maji kujaa mwilini na baadhi ya watu huvimba macho wakati wa asubuhi, ingawaje uvimbe huweza kupungua kwa baadaye.

Wengine hupata dalili za miguu kuvimba hasa asubuhi na kupungukiwa damu mwilini ambazo huweza kujitokeza kama dalili za kwanza..

Kama unasumbuliwa na matatizo yoyote ya figo unaweza kufika Mandai Herbalist Clinic kwani tuna dawa kwaajili ya kumaliza matatizo ya figo. Wasiliana nasi sasa kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment