Thursday, 4 June 2015

KUWA NA AFYA BORA NI JAMBO AMBALO HUSAIDIA KUWA NA UFANISI KATIKA KAZI . SASA LEO KUNA HIZI MBINU ZITAKAZOKUONGEZEA MOTISHA KATIKA KAZI YAKO

Kuna wakati mwingine baadhi yetu  huwa tunadhamira ya kufanya jambo fulani, lakini hujikuta tukiishia njiani kwa kukata tamaa.

Hivyo leo hii asubuhi napenda kukupa hizi njia chache ambazo zitakupa motisha kwa kile ambacho unataka kufanya au unakifanya kwa sasa.

Ni wazi kwamba bila kuwa na motisha hata utendaji wetu wa mambo mengi tunayofanya kila siku utakuwa ni mbaya au hafifu na siku zote matokeo ya kukosa motisha ni pamoja na kuwa na utekelezaji mbaya wa kazi zetu.

Mambo ambayo unapaswa kuyafanya ili kufanikisha mambo yako uliyojipangia katika kazi zako ni kama haya yafuatayo:

Kwanza kuwa na moyo wa kuthubutu kuanza, jilazimishe kuanza kufanya kitu ambacho umepanga kufanya hata kwa dakika chache tu. Kwa kufanya hivyo utaweza kujenga morali na nguvu ya kuendelea na kazi yako kama kawaida.

Achana na tabia ya kuwa na hofu au mawazo ya kushindwa, hii ni kwasababu kuwa na wasiwasi wa aina hiyo utakusababishia kupunguza ari ya kufanya jambo, lakini pia kuwa na hofu huweza kukusababishia kutomaliza mambo yako unayotegemea kukamirisha.

Mbinu nyingine ni kutafuta mtu wa kukupa motisha kila unapojisikia kuchoka au kukata tamaa.

Jitahidi pia kujitia moyo kwa kila hatua unayopiga katika mipango yako kazi au biashara zako, pendelea kujiuliza hili swali ‘Kama mtu mwingine ameweza basi hata wewe unaweza' Jiamini kuwa una uwezo mkubwa wa kufanya mambo vizuri zaidi kuliko mwingine yoyote ikiwa utatilia bidii unachotaka kitafanikiwa.

Penda kile unachokifanya, siku zote nguvu ya kufanya jambo lolote huletwa na chachu ya kuvutiwa na kitu fulani katika kazi.

Asante mdau wetu kwa kuendelea kufuatilia tovuti hii kila siku, tambua tunathamini sana uwepo wako wewe msomaji wetu popote pale ulipo. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia mawasiliano yafuatayo:0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment