Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 26 June 2015

LEO NI SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA SUALA LA UKOSEFU WA AJIRA NALO LIMETAJWA KUHUSIKA!!Afisa usalama wa nchini China akiandaa madawa ya kulevya yaliyokamatwa kwaajili ya kuyateketeza

Na Goodluck Ngowi.
Mwanza

Ikiwa leo Juni 26, ni siku ya maadhimisho ya kimataifa ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya, imefahamika kuwa moja ya  sababu zinazochangia vijana kujiingiza katika matumizi ya madawa hayo ni pamoja na ukosefu wa ajira.

Wakizungumza na mwandishi wetu wa tovuti hii jijini Mwanza baadhi ya vijana walioacha kutumia dawa za kulevya ambao kwa sasa wanaishi kwenye  nyumba maalumu  ya kurekebisha tabia yaani (Sober House) iliyopo  chini ya asasi isiyokua ya Kiserikali iliyopo katika Wilaya ya Ilemela mkoani humo

Gradious Faustine ni mmoja kati ya vijana walioacha kutumia madawa hayo alisema kuwa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi imekuwa ni moja ya chanzo kikubwa cha vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa hizo.

“Tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wengi  nchini pamoja na uelewa  mdogo juu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya ndiyo chanzo kinachochangia vijana kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya”  alisema Faustine.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Dawa za Kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko ameutaja mkoa wa Tanga kama kinara wa njia kuu za kusafirisha dawa hizo nchini, huku akisema kuwa  tangu mwaka 2010 ukamataji uliongezeka kutoka kilo 145 hadi kilo 813 mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 75.

“Kwa mujibu wa Ripoti mpya ya ofisi ya umoja wa mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu (UNODC)  imesema kuwa nchi ya Tanzania mji wa Tanga ndio kinara na njia kuu ya kusafirisha dawa za kulevya”  alisema Soko.

Maadhimishio ya siku hii ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya, yanatarajiwa kufanyika  kitaifa wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani, huku Rais Jakaya  Mrisho Kikwete akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Sasa wakati hayo yakiendelea hapa nyumbani Tanzania, huko nchini China wao hawana utani kabisa kuhusu hili la madawa ya kulevya yaani ukikamatwa nazo basi jua utakuwa na kazi ya ziada na wakizikamata uamuzi ambao hufanya ni kuzitekeza kabisa.

Tazama picha hizi 2 za haya madawa yalivyotekezwa baada ya kukamatwa nchini China..

Moto tayari umewashwa na madawa yanaanza kuteketea chini ya usimamizi wa maafisa usalamaMandai Herbalist Clinic tunasema kuwa kwa pamoja tukishirikiana kupinga matumizi haya ya madawa ya kulevya tutaweza kumaliza tatizo hili. Kikubwa kila mtu asimame katika nafasi yake katika kupambana na tatizo hili, huku tukiendelea kuwaunga mkono wale ambao tayari wameamua kwa dhati kuachana na matumizi ya madawa haya.

No comments:

Post a Comment