Tuesday, 23 June 2015

MAGONJWA MATANO YANAYOWEZA KUTIBIWA NA KIAZI MVIRINGO


Mara nyingi tumekuwa tukitumia viazi mviringo kama chakula ambacho huweza kupikwa au kutengenezwa kwa namna mbalimbali kutokana na uhitaji wa mhusika.

Mtaalam wa tiba asili Dk Abdallah Mandai kutoka Mandai Herbalist Clinic anasema kuwa, viazi hivyo vikipondwa na kubandikwa juu ya tatizo lolote la ngozi au bawasira huwa tiba nzuri sana.

Aidha, juisi ya kiazi kilichopondwa ni nzuri sana kwa matatizo kama baridi yabisi, vidonda vya tumbo, asidi ya tumboni.


Pia viazi hivyo, husaidia kwa wale wenye matatizo ya jongo (gout) na huondoa sumu mwilini (antidote, acidosis), huku kiazi cha kijani sana kikiwa na chembe chembe fulani za sumu zijulikanazo kama vile 'solanine’inayoathiri sehemu ya via vya uzazi.

Hali kadhalika, kiazi pia ni ‘tonic’ nzuri sana ya ngozi, kinachotakiwa kufanyika katika hili ni kunawia juisi yake na machicha yake utayabandika kila mahali juu ya ngozi na itasaidia kuondoa makunyanzi yote ya uzee pamoja na kulainisha ngozi.

Kwa ushauri zaidi unaweza kufika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege, jijini Dar es Salaam au tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.

No comments:

Post a Comment