Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Tuesday, 30 June 2015

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YAZIDI KUWA TISHIO NCHINI


Imeelezwa kwamba magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo, kisukari na saratani yamezidi kuongezeka kwa kasi na kuendelea kuwa chanzo cha vifo duniani.

Hayo yalisema jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Huson Rweumbiza, wakati wa semina ya siku moja iliyowashirikisha waandishi wa habari. Ambapo Rweumbiza alisema kuwa hapa nchini Tanzania takribani watu tisa kati ya mia moja wana ugonjwa wa kisukari, huku mtu mzima mmoja kati ya watatu ana tatizo la shinikizo la juu la damu.

Rweumbiza alisema kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Taasisi ya Kisukari Tanzania na wadau wengine imeandaa kitabu kwa lengo la kupunguza madhara ya matokeo mapya ya magonjwa yasiyoambukizwa ndani ya jamii ya Watanzania.

Akifafanua kuhusu kitabu hicho, amesema kuwa kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha nyepesi na kinajumuisha taarifa muhimu, huku kikimpa nafasi kila mtu kuchagua mtindo wa maisha utakaomwezesha kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa usioambukizwa.

Mbali na hayo, Rweumbiza amewataka wananchi kuacha kuamini uzushi ulizuka mitaani kuwa mayai ya kware hutibu ugonjwa wa kisukari, shinikizo la damu na kuongeza kinga kwa watu wenye UKIMWI.

“Watu wapo kibiashara zaidi mayai yak ware ni kama mayai ya kuku na bata na hayatibu kisukari, shinikizo la damu wala kuongeza kinga kwa watu wenye UKIMWI,” alisema Rweumbiza

Kisukari pekee yake kinakadiriwa kuathiri maisha ya watu takribani milioni 371 duniani kote, huku asilimia 80 ya idadi hiyo ikiishia katika nchi zenye uchumi wa kati na masikini.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment