Tuesday, 23 June 2015

MAJANGA YA NCHI KUKUBWA NA JOTO KALI YAMEENDELEA DUNIANI SASA NI ZAMU YA PAKISTANIKatikati ya mwezi Mei mwaka huu nchi ya India ilipata pigo baada ya kupoteza zaidi ya watu 800 kutokana na kuongezeka kwa joto lililofikia nyuzi joto 48.

Mwezi Juni imekuwa kama ni zamu ya nchi ya Pakistani ambapo unaambiwa kuwa mpaka sasa watu 700 wamefariki kutokana na ongezeko la joto lililofikia nyuzi joto 45.

Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa mara moja ili kukabiliana na hali hiyo.

Raia wa nchi hiyo wakijinusuru kwa kuogelea kwenye mito
Hadi sasa tayari Jeshi limepelekwa katika eneo la Kusini mwa mji wa Karach ambako idadi kubwa ya vifo imetokea na kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura.

Imeelezwa kuwa watu walioathirika zaidi ni watu wazima ambao wana kipato cha chini, huku wengine wakiwa katika hali mbaya.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa maelezo zaidi au ushauri, piga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment