Friday, 5 June 2015

MAJANI YA MWEMBE NAYO KWETU NI TIBA


Muembe ni mti unaotoa matunda yaitwayo maembe, ambayo huwa na ladha nzuri, lakini mbali na mti huu kutupatia matunda pia unaweza kutumika zaidi na kuwa dawa ya matatizo mbalimbali.

Majani ya mti wa mwembe yanapochemshwa huweza kutumika kama tiba ya matatizo haya yafuatayo;

Husaidia sana kuweza kutibu wale wenye tatizo la kikohozi kikavu.

Aidha, maji yake huweza kusaidia katika kuoshea vidonda kimsingi majani ya mwembe yanauwezo mkubwa wa kukausha majeraha.

Pia husaidia sana kutoa ahueni kwa wale wenye matatizo ya pumu.

Mbali na hayo, unga wa majani ya mwembe huweza kutumika kwa kutunza meno , ambapo mtu mwenye tatizo hilo atapaswa kusukutua kwa kutumia unga unaotokana na majani hayo.

Kama ungependa kuuliza zaidi au kupata ushauri kutoka kwetu Mandai Herbalist Clinic basi wasiliana nasi kwa simu namba: 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment