Tuesday, 23 June 2015

MANDAI HERBALIST CLINIC YATOA MSAADA KWA KIKUNDI CHA SANAA


Mandai Herbalist Clinic iliyopo Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam jana Juni 22, 2015 ilitoa msaada wa nguo aina ya track suit na T.shirt. kwa kikundi kiitwacho Mongolandege Sanaa Group.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mbele ya mwenyekiti wa mtaa huo wa Mongalandege, Mkurugenzi Mkuu wa Mandai Herbalist Clinic, Tabibu Abdallah Mandai amesema kuwa kutokana na kupokea maombi ya kikundi cha Mongolandege Sanaa Group ameamua kutoa jezi hizo aina ya Track suit na T.shirt ambazo anaamini zitawasaidia sana katika sanaa ya kikundi hicho.

Aidha, Tabibu Mandai amesema kuwa miongoni mwa maombi ya vifaa alivyoombwa ilikuwa ni pamoja na jezi,  Track suit na mipira.

"Bahati nzuri leo tumeweza kupata vifaa vya aina mbili yaani track suit na jezi, ambazo hii leo tunamkabidhi Mwenyekiti kisha mwenyekiti atawakabidhi vijana na tunaahidi tutaendelea kuwasaida zaidi pale ambapo tutakuwa na uwezo wa kuwasaidia." alisema Dk Mandai.

Tabibu Mandai aliongeza kuwa, " leo tumependa kuanza kubadilisha muonekano wao kama walikuwa wakivaa kila mmoja kivyake vyake basi sasa itakuwa ni sare kwa wanakikundi wote."

Wanakikundi wa Mongolandege Sanaa Group wakipeana mikono na Mwenyekiti wa mtaa wa Mongolandege (katikati) mara baada ya kukabidhiwa msaada wao.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga Ndugu, Iddi Seleman Kilindi amesema kuwa anashukuru kwa uzalendo wa Dk Mandai ambao amekuwa akiuonesha katika masuala mbalimbali ya kijamii na kusema kuwa katika mtaa huo kuna watu wengi wenye uwezo na kufanya shughuli mbalimbali mtaani hapo, lakini wengi wao wamekuwa hawaikumbuki jamii na kuisaida.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa mtaa wa Mongolandege kata ya Ukonga Ndugu, Iddi Seleman Kilindi (kushoto)akimkabidhi Mkurugenzi wa Kikundi cha Mongolandege Sanaa Group Seveline Daudi moja ya Track Suit zilizokabidhiwa kwao na Mandai Herbalist Clinic
"Mimi napenda kuwaambia wadau wengine wajitolee kuwasaidia vijana katika masuala haya ya sanaa kwani nayo kwasasa imekuwa kama ajira kwa vijana." Alisema Mwenyekiti Seleman

Mbali na  hayo, mwenyekiti huyo amesema kuwa kufuatia msaada huo anaamini hata vijana wataongeza juhudi zaidi katika sanaa yao.
Wanakikundi wa Mongolandege Sanaa Group katika picha ya pamoja
"Msaada huu nadhani utawafanya vijana kuongeza juhudi zaidi katika masuala  ya sanaa ili kuhakikisha kikundi chao kinakwenda mbele zaidi." alisema Mwenyekiti.

Wanakikundi wakionesha moja ya T. Shirt waliyopokea kutoka Mandai Herbalist Clinic
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kikundi cha Mongolandege Sanaa Group Seveline Daudi, amesema kuwa kikundi hicho kimekuwa na dhamira ya kuwakomboa vijana katika sanaa na kumshukuru sana Tabibu Mandai kwa msaada wake aliowapati.

Kumbuka kuwa Mandai Herbalist Clinic imetoa Track Suit 30 na T.shirt 30 kwaajili ya matumizi ya kikundi hicho cha Mongolandege Sanaa Group

No comments:

Post a Comment