Monday, 15 June 2015

MAZIWA MTINDI YANASIFAKA SANA KWA KUWA NA VIRUTUBISHO VINGI, LAKINI JE, UNAJUA NI NCHI GANI INAONGOZA KWA MAUZO YA MAZIWA HAYO?Maziwa mtindi ni moja ya maziwa yenye virutubisho vingi sana mwilini.

Nchi nyingi zimekuwa zikisindika maziwa hayo na moja ya nchi ambazo zinaelezwa kuzalisha maziwa hayo kwa wingi ni Uturuki.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015, mauzo ya mtindi nje ya nchi yamechangia kiasi cha dola milionii 12 katika uchumi wa Uturuki.

Mauzo hayo ya mtindi katika robo ya kwanza ya mwaka 2015 yamevunja rekodi ya mauzo ya robo ya kwanza ya mwaka 2014

Kwa mujibu wa takwimu za biashara za nje, zinaonesha kuwa takribani tani 191,299 za mtindi zimezalishwa kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka huu zikizipita tani 189,129 za mwaka jana.

Mauzo ya mtindi yamechangia takriban dola milioni 12 katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.

Uturuki imekua ikiuza bidhaa hiyo kwa nchi 16 sasa zikiwemo Marekani, Iran, Iraq, Quwait na Singapore.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.  

No comments:

Post a Comment