Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Friday, 26 June 2015

MBEGU ZA KIUME ZIMESHAURIWA KUVUNWA HASA ZILE ZA VIJANA WENYE UMRI WA MIAKA 18 ILI ZITUMIKE KUPANDIKIZIA WANAWAKE.


Je, umewahi kuwaza kuhusu hili la mbegu za kiume kuvunwa?

Sasa imeelezwaa kwamba ni vyema mbegu za uzazi wa wanaume zikavunwa na kuhifadhiwa mara tu pale mtu anapotimiza miaka 18.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtafiti wa maswala ya uzazi nchini Uingereza Daktari Kevin Smith, amesema kuwa manii ya mwanaume huwa katika hali bora zaidi wakati wa umri huo na hivyo mbegu zinapaswa kuvunwa na kisha kutumika kupandikiza wanawake katika siku za usoni.

Daktari Smith, ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo kikuu cha Abertay kilichoko Dundee nchini Uingereza amesema kuwa baada ya utafiti wa kipindi kirefu amebaini kuwa ni bora kuvuna manii mapema ili kuepuka maradhi mengi yanayochangiwa na kuongezeka kwa umri.

Dk. Smith, anasema kuwa Wizara ya Afya ya Uingereza inapaswa kuunda hifadhi maalum ya mbegu za uzazi ili kupunguza visa vya maradhi aliyoorodhesha.

Pamoja na maoni hayo ya Dk. Smith. Wauguzi wa masuala ya uzazi wameonekana kupinga jambo hilo na kusema kuwa njia hiyo haitakuwa suluhishi la kudumu.

Dk. Kevin Smith
Mbali na hayo, akitetea wazo lake katika jarida la madaktari la ''The Journal of Medical Ethics, Dakta Smith amesema kuwa wale wanaotaka kupata watoto mapema basi wafanye hivyo, lakini kwa wale ambao wamegonga miaka 40 ni vyema watumie mbegu walizohifadhi kwa matokeo mazuri zaidi.

Takwimu zinaonesha kuwa wanaume wanaanza kupata watoto wakiwa na umri wa miaka 33 ikiwa ni ongezeko kutoka kwa miaka 31 katika miaka ya tisini, lakini mwanasayansi Sheena Lewis, aliwashauri wanaume waanze kushughulikia swala la familia mapema katika ujana wao.

''Ninataka kuwaelezea wazi kuwa umri mzuri wa kuzaa kwa wanaume na wanawake ni kati ya miaka ya 20 na 30." Alisema mwanasayansi Lewiis.

Ndugu yangu kama unateseka na magonjwa mbalimbali ni vyema ufanye utaratibu wa kuwahi kufika Mandai Herbalist Clinic sasa ili upate suluhisho la matatizo yako ya kiafya. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment