Thursday, 11 June 2015

MGOMBEA URAIS MKULIMA MWENYE DHAMIRA YA KUONGOZA NCHI


Eldeforce Bilohe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu
Tumeshuhudia makada mbalimbali wakiwemo viongozi wakubwa wa nchi na maarufu kutoka Chama cha Mapindizi CCM wakitangaza nia zao za kuwania kiti cha urais.

Zoezi hilo liliendelea hapo jana ambapo Mkulima kutoka Kasulu mkoani Kigoma Eldeforce Bilohe (43) naye alichukua fomu ya kuwania urais na kusema kuwa kati ya wagombea 27 ambao wameshajitokeza haoni kama kuna mgombea ambaye ni tishio kwake.

“Kati ya wagombea 27 ambao tayari wamechukua fomu kabla yangu sioni kama kuna mgombea tishio kwangu,” alisema mgombea huyo huku akishangiliwa.

Akizungumza juu ya azma yake hiyo, mgombea huyo alisema ameamua kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani amekuwa na dhamira hiyo tangu mwaka 2003.

Aliongeza kuwa “Dhamira hiyo iko moyoni tangu mwaka 2003 pale ambapo nilipotaka kuweka mambo sawa baadhi ya mambo yalijitokeza na kuchelewesha kusudio hilo,” alisema.

Hata hivyo, pamoja na kusema kuwa na dhamira hiyo kutoka moyoni, mgombea huyo alishindwa kueleza vipaumbele, huku akisema kuwa ajira kwa vijana na maisha bora kwa wastaafu.

Akielezea alipopata fedha za kuchukuwa fomu hiyo ya urais alisema fedha zimetoka mfukoni mwake na hajachangiwa na mtu yeyote .

Aidha, mgombea huyo yeye hakuongozana na mke wake na alipoulizwa alisema kuwa kwa sababu ambazo hazijaweza kuzuilika, mkewe alimtaka atangulie lakini pale atakapohitajika atapatikana.

Mbali na hayo yote, mgombea huyo wakati akizungumza alisahau kuzima simu yake na ikaita kisha akaamua kuipokea.

“Subiri kidogo,” aliongea na simu kisha akakata.

 Shukrani kwa kuichagua tovuti hii kujipatia taarifa mbalimbali, lakini kumbuka kuwa ikiwa unasumbuliwa na magonjwa sugu Mandai Herbalist Clinic tupo kwaajili yako tunapatikana Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam . Tiba zetu ni za asili zitokanazo na mimea, matunda, nafaka, na mitishamba. tupigie kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail.

No comments:

Post a Comment