Monday, 22 June 2015

MLIPUKO MKUBWA WAZUA TAHARUKI KARIBU NA BUNGE LA AFGHANISTAN

Bunge la Afghanistan
Mara nyingi katika ofisi za serikali huwa kuna kuwa na ulinzi mkubwa na miongoni mwa sehemu ambazo huendesha shughuli za kiserikali na huhitaji ulinzi mkubwa pia ni pamoja na Bunge.

Lakini huko nchini Afghanistan leo kuna ripoti ya kuwepo kwa mlipuko mkubwa karibu na bunge la nchi hiyo huko Kabul .

Kufuatia tukio hilo picha za runinga zimeonesha wabunge wakikimbilia usalama wao,  huku kukiwa na taarifa zinazosema kuwa watu waliokuwa na bunduki walivamia jengo hilo.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa Polisi wanajaribu kuwaondoa watu katika eneo hilo.

Endelea kuwa karibu na tovuti hii kwa ajili ya kufikiwa na taarifa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment