Friday, 12 June 2015

MLONGE UMEENDELEA KUPATA SIFA ZAIDI DUNIANI KUTOKANA NA UWEZO WAKE WA KUTIBU MAGONJWA


Mlonge ni mmea ambao umekuwa ukisfika sana kutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa mbalimbali yanayotusibu binadam.

Leo nina hii taarifa kutoka nchini Togo, Afrika Magharibi ambapo mmea wa mlonge umetambuliwa na Kongamano la Umoja wa Mataifa la Misitu (UNFF) kutokana na manufaa yake katika lishe ya binadam.

Majani ya mti huu yameelezwa kuwa na faida nyingi za kiafya, na umeelezwa kuwa na vitamin nyingi zenye uwezo wa kuimarisha mwili.

Mlonge ni mti ambao umeelezwa kustawi haraka na hauhitaji maji mengi ili kustawi kwake, huku ukiwa na manufaa mengi kwa familia kutokana na uwezo wake wa kupunguza utapiamlo.

Nchini Togo, mmea huu bado haujulikani sana, lakini kilimo chake kimeanza kunufaisha baadhi ya wakulima.

Mmoja mwa wakulima wa mlonge nchini Togo, Adevid Komnaerick ambaye anashamba la heka tatu la miti hiyo ya mlonge anasema kuwa “nyumbani kwangu mke wangu na mtoto wangu sote tunapenda kula mchuzi wa mlonge tangu mtoto wangu wa kiume alipozaliwa nimekuwa na mpa mlonge kila siku nimeona ameanza kuwa na akili na nguvu kwa kila kitu anachofanya imeimarisha sana afya ya familia yetu nzima.”

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment