Saturday, 6 June 2015

MSIMU WA MACHUNGWA NDIO HUU, NI VYEMA TUKUMBUSHANE HIZI FAIDA CHACHE ZA TUNDA HILIChungwa ni moja ya tunda ambalo linafahamika sana miongoni mwa watu wengi , lakini pia tunda hili lina ladha nzuri.

Leo nimeona nikupe hizi faida utakazozipata pale unapotumia tunda hili la chungwa.

Chungwa huweza kumsaidia mtumiaji kujenga mifupa ya meno, hii ni kwasababu chungwa huwa na kiasi kingi cha madini ya calcium abayo husaidia kuimarisha mifupa hiyo ya meno.

Husaida sana kuimarisha kinga ya mwili kutokana na kuwa na vitamin C ambayo husaidia uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu mwilini kwa sababu ya kuimarisha kinga za mwili.

Chungwa pia husaidia afya ya ngozi, hii ni kwasababu ndani ya chungwa huwa kuna ‘anti oxidants’ ambayo hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya ngozi, lakini pia huifanya ngozi kutozeeka mapema.

Matumizi ya machungwa hufaa zaidi kwa wale wenye shida ya shinikizo la juu la damu yaani (high blood pressure) hivyo kimsingi machungwa ni mazuri kwa wenye matatizo ya presha.

Mbali na hayo, pia kwa wale wenye shida ya ukosefu wa choo (consumption) chungwa husaidia pia kutokana kuwa na nyuzinyuzi yaani ‘fiber’ hivyo nyuzinyuzi hizo husaidia sana katika usagaji wa chakula tumboni na hutoa ahueni zaidi kwa wale ambao tayari wana tatizo la kukosa choo.
  
Hizo ni faida chache ambazo nimeona ni vyema upate kuzifahamu leo kutoka Mandai Herbalist Clinic kwa ushauri na maoni zaidi unaweza kuwasilina nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment