Wednesday, 3 June 2015

MTALII AFARIKI BAADA YA KUJERUHIWA NA SIMBA KISA ALIKAIDI MAELEKEZO YA MBUGANI


Mara nyingi unapotembela sehemu za mbuga za wanyama huwa kunakuwa na maelekezo ambayo watalii hupatiwa kabla ya kuingia kutalii na pale unapokaidi maelekezo hayo basi huenda kikatokea kama hiki kilichotokea Afrika Kusini

Mwanamke mmoja wa Marekani aliyekuwa akitalii mbuga ya wanyama ya Lion Park iliyoko mjini Johannesburg, ameripotiwa kufariki baada ya kushambuliwa na simba.

Mwanamke huyo inaelezwa alikuwa akiendesha gari mbugani humo huku kioo cha dirisha la gari lake kikiwa wazi na kupuuza ishara za onyo zilizokuwa zimewekwa katika mbuga hiyo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni msimamizi hiyo bwana Scott Simpson alisema kwamba aliona simba akimshambulia mwanamke huyo kupitia dirisha lililokuwa wazi katika upande wa kiti cha abiria.

Hata hivyo wahudumu wa mbugani hiyo walikwenda kumsaidia mwanamke huyo, lakini alifariki walipokuwa wakijaribu kumptia matibabu.

Aidha, msimamizi huyo Simpson aliarifu kwamba ndani ya mbuga hiyo kuna mabango 40 ya ishara yaliyoandika kwa maneno na picha zinazoonesha watalii kutofungua vioo vya madirisha na kutoka nje ya magari yao wanapokuwa wakitalii.

Pamoja na hayo imeelezwa kuwa simba huyo aliyemshambulia mtalii amehamishiwa na kufungiwa katika eneo lisilokuwa wazi kwa watalii.


Asante kwa kuendelea kutembelea tovuti hii na kuifanya moja ya sehemu yako ya kuhabarika juu ya masuala mbalimbali.

No comments:

Post a Comment