Wednesday, 10 June 2015

MWANAMKE WA KWANZA DUNIANI KUJIFUNGUA MTOTO KWA NJIA YA KUWEKA MAYAI KWENYE JOKOFU

Mwanamke mmoja nchini Ubelgiji amekuwa wa kwanza duniani kujifungua mtoto kwa kutumia upandikizaji wa mayai ya mwanamke yaliowekwa katika jokofu alipokuwa mtoto.

Msichana huyo wa miaka 27 alikuwa na mayai yaliotolewa akiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kuanza kupewa matibabu ya anemia ya seli.

Mayai yake yaliyosalia yalifeli kutokana na matibabu hayo hatua ambayo ingeathiri uwezo wake wa kushika mimba bila upandikizaji huo.

Mwanamke huyo alijifungua mvulana mwenye afya nzuri mwezi Novemba mwaka 2014 na maelezo kuhusu swala hilo yalichapishwa siku ya jumatano katika jarida la kizazi cha binaadamu.

Mwanamke huyo ambaye hakutaka kujulikana alipatikana na ugonjwa wa anemia ya seli alipokuwa na umri wa miaka mitano.

Wataalam wanatumai kwamba mpango huo huenda ukawasaidia wagonjwa wengine wadogo.

Shukrani kwa kuendelea kuwa karibu nasi mdau wetu, lakini kumbuka ukiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali Mandai Herbalist Clinic ipo kwaajili yako. Tunatoa tiba zetu kwa njia ya mimea tiba, nafaka na matunda. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment