Friday, 12 June 2015

MWANAMUME ALIYEPANDIKIZWA UUME ANATARAJIA KUWA BABA HIVI KARIBUNI!!


Madaktari wakiwa katika chumba cha upasuaji
Daktari wa usapuaji nchini Afrika Kusini amethibitisha kwamba mwanaume wa kwanza aliyepandikizwa uume atakuwa baba hivi karibuni.

Professor Andre van der Merwe, ambaye ndiye aliyefanya upasuaji huo mwezi Disemba, ameiambia BBC kwamba mwenza wa mgonjwa huyo ana uja uzito wa miezi minne.

Mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 21 alipoteza uume wake pindi alipokuwa anapashwa tohara ambayo haikufanikiwa.

Professor van der Merwe ameendelea kusema habari hizo zinaonyesha kuwa upandikizwaji huo wa kiungo umefanikiwa kabisa na unaweza kufanyiwa wagonjwa wengine katika siku zijazo.

Endelea kuwa karibu nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka tovuti hii ya www.dkmandai.com, lakini inapofika wakati utajisikia haupo vizuri kutokana na kuumwa basi wasiliana nasi Mandai Herbalist Clinic kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment