Friday, 5 June 2015

MZEE HUYU ANASEMA ALIZINGATIA MASUALA YA MLO ASILIA NA SASA ANAMIAKA 102 NA BADO YUPO FITI


Kushoto ni Mzee Said Issa Khamis mwenye umri wa miaka (102) kulia ni mtoto wake wa mwisho Fatuma Said Issa aliyezaliwa mwaka 1962.
Katika maisha tunayoishi kila mtu angetamani kuishi maisha marefu zaidi hapa duniani, lakini kwa bahati mbaya sana hali ilivyo kwa miaka ya sasa wengi huwa tunaishia umri wa katikati tu si kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Miaka ya nyuma wazee wetu walikuwa wakibalikiwa na mwenyezi Mungu kuishi maisha marefu sana na walikuwa wakiishi wakiwa na afya bora iyokuwa na kupata misukosuko ya magonjwa ya hapa na pale.

Hali kwa sasa ni tofauti sana wengi wanafariki wakiwa bado na umri mdogo, lakini wiki hii Kitengo cha Habari kutoka Mandai Herbalist Clinic kilitembelewa na mzee aitwaye Said Issa Khamis (pichani hapo juu) ambaye yeye anaumri wa miaka 102  hadi sasa na anadai kuwa yupo vizuri bado kiafya.

Kitengo chetu cha habari tukitaka kushare naye mambo machache namna yeye alivyokuwa akiishi tangu enzi za ujana wake hadi kufikia umri huo.

Ambapo mzee Khamis anaanza kwa kukiri kuwa yeye enzi za ujana wake alikuwa ni mvutaji mkubwa wa sigara, lakini ghafla tu alijikuta ameanza kuichukia sigara na baadaye alifanikiwa kuacha kabisa kutumia.

Mzee Khamis anasema kuwa kwa kile kipindi chote ambacho alikuwa akivuta sigara, hakuwahi hata mara moja kunywa pombe ya aina yoyote kitu ambacho huwa anafikiri huenda kimemsaidia kuishi maisha marefu kiasi hicho.

Aidha, mzee Khamis alipohitajika kutuelezea namna mpangilio wa mlo wake ulivyo alisema kuwa " mimi na familia yangu tangu enzi hizo tumekuwa tukitumia sana ugali wa muhogo pamoja na mbaoga za majani mara kwa mara kuliko vyakula vingine na ilipobidi kubadili mboga basi tulitumia samaki zaidi."

Mzee Khamis anaendelea kueleza kuwa " nyama kwetu haikuwa na kipaumbele kwa kweli ilikuwa inaweza kupita hata mwaka hatujala nyama sisi ilikuwa ni samaki tu"

Akielezea kuhusu mlo wake wa asubuhi mzee Khamis anasema kuwa " mimi kwa kawaida nikiamka asubuhi jambo la kwanza ni lazima ninywe maji glasi moja na hii tabia ya kunywa maji sikufundishwa na mtu nilijiwekea tu mimi mwenyewe huo utaratibu".

"Baada ya kunywa glasi moja ya maji naweza kufanya baadhi ya shughuli zangu chache asubuhi kisha nakunywa chai inawezekana na magimbi, mihogo ya kuchemsha, viazi vitamu vya kuchemsha, huu ndio naweza sema ulikuwa utaratibu wangu." alisema mzee Khamis.

Kushoto ni mzee Said Issa Khamis akiwa na binti yake Fatuma Said Issa binti yake huyo alizaliwa mwaka 1962


Mbali na hayo mzee Khamis amesema kuwa "hata haya baadhi ya magonjwa yanayoibuka siku hizi kwa kiasi kikubwa ni kutokana na vyakula vijana wanavyokula na ndio wanavipenda kweli".

Aliongeza kuwa "Mimi nawashauri wapendelee kula ugali wa dona au wa muhogo pamoja na mboga za majani watakuwa imara na nguvu pia na kuishi maisha marefu zaidi kwani bado hawajachelewa."

Mzee Khamis ni mkazi wa jijini Dar es Salaam maeneo ya Mbagala, Charambe alikuwa na watoto 7, lakini bahati mbaya wengine walifariki na amebaki na watoto wawili mmoja kati ya hao wawili waliobaki ndio alikuwa amemleta kwetu Mandai Herbalist Clinic kwaajili ya matibabu  na anadai bado yupo vizuri tu na yeye ndiye anailisha familia yake hadi sasa.

Unaweza kuwasilina nasi kwa namba za simu zifuatazo 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment