Saturday, 20 June 2015

MZEE MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI AFARIKI

Mzee Jeralean Talley mwenye umri mkubwa dunia wa miaka 116 afariki dunia.

Mzee huyo ambaye ni raia wa Marekani alipata fursa ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa mwezi mmoja uliopita kabla ya kifo chake.

Talley, amefariki akiwa nyumbani alipokuwa akiishi na mdogo wake Detroit.

Mdogo wake ambaye naye ana umri wa miaka 77 alisema kuwa Talley, alikuwa mtu mwema na atakumbukwa kwa mazuri yake.

Talley, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji mapafuni ambapo alipelekwa hospitali na baadae kuruhusiwa na mauti kumkuta akiwa nyumbani.

Shukrani kwa kuendelea kupitia tovuti hii mara kwa mara, tambua tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu, tunaomba uendelee kuwa nasi kila siku kwaajili ya kupata taarifa mbalimbali 

No comments:

Post a Comment