Wednesday, 10 June 2015

NAMNA YA KUKABILIANA NA UGONJWA WA KISUKARIWatu wengi wenye kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari hujikuta katika changamoto kubwa pale inapofika hatua ya kusishi na ugonjwa huo.

Wengi hupata tabu zaidi katika masuala ya mpangilio ya mlo, lakini kimsingi ni muhimu sana kuwa na uwiano mzuri katika mpangilio wa mlo na kuzingatia mazoezi ili kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu.

Unapokuwa na ugonjwa huu hukulazimu kubadili mtindo wako wa maisha ya kila siku

Kuna baadhi ya mambo ambayo ni vyema ukayazingatia unapokuwa unasutatizo la kisukari ambayo ni pamoja na kuchagua aina ya chakula na kiasi utakachokula kila siku, kupima kiwango cha sukari yako mwilini mara kwa mara, kufanya mazoezi, kuhudhuria kliniki ya sukari kama umeanza pamoja na kutumia dawa zako kwa mujibu wa maelekezo uliyopatiwa na daktari wako.

Tunapozungumzia mlo ni vizuri ukapenda kula vyakula tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na mboga za majani, nafaka zisizokobolewa, epuka kula chakula cha aina moja kila siku pia jaribu kula kila baaada ya muda.

Mbali na hayo, zingatia sana suala la kufanya mazoezi kwani ni sehemu muhimu ya kudhibiti ugonjwa wa kisukari kwababu mazoezi husaidia kupunguza kiasi cha glukozi kilichipo kwenye damu. Unaweza kufanya mazoezi ya kutembea, kukimbia au kuendesha baiskeli fanya hivyo angalau dakika 30 kila siku.

Mandai Herbalist Clinic pia tunayo dawa nzuri kwa wenye shida ya kisukari wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. Karibu.

No comments:

Post a Comment