Tuesday, 16 June 2015

NIMEKUKUSANYIA PICHA NA MATUKIO MBALIMBALI KUTOKA OFISI ZA BAKWATA LEO KATIKA ZOEZI LA KUMUOMBEA DUA MUFTI SHEIKH ISSA SHAABAN BIN SIMBA


Wakati mwili wa Mufti na Shehe Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba aliyefariki dunia jana asubuhi ukitarajiwa kuzikwa leo jioni mkoani Shinyanga, wananchi na viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa wamejitokeza jijini Dar es Salaam katika ofisi za BAKWATA makao Makuu iliyopo Kinondoni Muslim kwaajili ya kumuombea dua Mufti na Sheikh Simba

Katika dua hiyo ambayo imehudhuriwa na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilali,  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi pamoja na viongozi wengine akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mheshimiwa Muhammed Aboud, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha wananchi Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, (CUF) .

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilali
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa,

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mheshimiwa Muhammed Aboud akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika ofisi za BAKWATA leo


Mwenyekiti wa Chama cha wananchi  (CUF) Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, .mara baada ya kuwasili katika eneo la ofisi za BAKWATA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumaza na waandishi wa habari kuhusu msiba wa Mufti na Sheikh Issa Bin Shaaban Simba  Wengine waliohudhuria pia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema na Mwana siasa mkongwe nchini Kingunge Kombale - Mwilu,  


Mwana siasa mkongwe nchini Kingunge Kombale - Mwilu alipokuwa akiwasili katika ofisi za BAKWATA

Kushoto Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema
Mkurugenzi Mkuu wa IPP Media Dk Reginald Mengi akizungumza na wanahabari katika viwanja vya ofisi za BAKWATA
Baadhi ya watu waliojitokeza katika viwanja vya BAKWATA leo
Katikati ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akiongea na wanahabari kuhusu msiba wa Mufti na Sheikh Issa Bin Shaaban Simba
Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya familia, Mufti alifikwa na mauti akiwa katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu


  

No comments:

Post a Comment