Tuesday, 16 June 2015

NINAPENDA KUKWAMBIA HAYA MACHACHE KUHUSU ZABIBU NA FAIDA ZAKE.Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.

Matunda haya hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.

Zabibu husaidia kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Matunda haya pia husaidia damu kuwa nyepesi na kuzuia isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo kutokana na sababu hii hupunguza hatari ya kukubwa na kiharusi (stroke)

Zabibu pia inasaidia kuzuia na kutibu tatizo la upungufu wa damu na kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.

Hali kadhalika, haya husaidia katika kutibu na kutoa kinga ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za kueleweka au za moja kwa moja.

Juisi yake husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi vizuri na kuzuia ukavu wa haja kubwa.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment