Tuesday, 9 June 2015

NYUKI WASABABISHA KUAHIRISHWA KWA SAFARI YA NDEGE KWA ZAIDI YA SAA MBILI


Abiria wa ndege moja ya shirika la ndege la Flybe linalohudumu nchini Uingereza wamejikuta wakicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili baada nyuki kuingia ndani ya mitambo ya ndege hiyo.

Inaelezwa kuwa wahandisi wa ndege hiyo walibaini kuwa nyuki huyo alipenyeza na kuingia ndani ya mitambo ya ndege hiyo na hivyo safari haingewezekana. Hivyo kuwalazimu wahandisi hao kutafuta mbinu za kumtoa mdudu huyo.

Ndege hiyo ya Flybe yenye namba ya usajili BE384 iliyokuwa ikitoka Southampton kuelekea Dublin.

Abiria mmoja aliyekuwa ndani ya ndege hiyo Noel Rooney, anasema hakuamini tukio hilo hasa kwani ndege hiyo imeitwa jina la nyuki!

Taarifa kutoka kwa shirika hilo lilisema kuwa nyuki huyo alikuwa ndani ya mitambo muhimu ambayo ingehatarisha maisha ya abiria wake.

''Rubani wetu alitahadharishwa na kuwepo kwa nyuki na akalazimika kurejea mara moja katika uwanja wa ndege wa Southampton'.' Nyuki huyo alikuwa ndani ya mitambo muhimu ambayo ingehatarisha maisha ya abiria wake.

Hata hivyo, shirika hilo limewaomba radhi abiria wote waliokerwa na hatua ya kurejea kwa ndege hiyo.

Asante kwa kutembelea www.dkmandai.com, lakini kama unasumbuliwa na magonjwa sugu unaweza kuonana na Tabibu Mandai kwa kufika ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam, au piga simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment