Saturday, 13 June 2015

ORODHA YA VYAKULA AMBAVYO VINAWEZA KUKUSAIDIA UNAPOPATWA NA MAFUA


Mafua ni ugonjwa ambao husumbua watu wengi , ugonjwa huu mara nyingi huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa.


Ugonjwa huu ni nadra sana kuwapata wale ambao wanakinga ya kutosha katika miili yao.


Vyakula vifuatavyo vinauwezo mkubwa wa kuimarisha kinga ya mwili na kupambana na maambukizi.


Kitunguu swaumu kina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza.


Unaweza kutumia kitunguu swaumu kwa kupika kwenye chakula au kwa kutafuna punje za kitunguu swaumu.


Pia ulaji wa vyakula vyenye vitamin C kwa wingi husaidia sana kuzuia na kuondoa ugonjwa wa mafua.


Miongoni mwa vyakula vyenye vitamin C ni pamoja na mboga za majani na matunda kama machungwa.

Ikiwa unasumbuliwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo sugu ni vyema ukafanya uamuzi sahihi wa kufika Mandai Herbalist Clinic ili kuonana na Tabibu Abdallah Mandai na kuweza kupata matibabu sahihi. Unaweza kupiga simu namba; 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika moja kwa moja ofisini Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment