Thursday, 25 June 2015

PATA UFAHAMU KUHUSU UPEKEE WA TUNDA LA KOMAMANGA KATIKA MASUALA YA TIBA


Habari mpenzi msomaji wa tovuti yetu ya www.dkmandai.com natumaini mzima wa afya. Bado tunaendelea kupeana mambo mengi mazuri ambayo pengine huyajui au unayajua kwa uchache.

Leo tunapenda kulielezea tunda la komamanga na faida zake mwilini.

Kwanza kabisa tunda hili lina asili ya nchini India, lakini kwa jina la kisayansi hufahamika kama 'Punica Granatum.'

Tunda hili hustawi sana kipindi cha mwezi wa pili na mwezi wa tisa, na huweza kushamiri sana katika hali ya hewa ya joto. Pia mmea wa tunda hili unasifika kwa uwezo wake wa kumudu hali ya ukame.

Virutubisho vinavyopatika katika komamanga ni pamoja na vitamin C kwa wingi Vitamin B5 Vitamin A Vitamin E madini kama Potassium na madini chuma.

Aidha, mbegu za tunda hili ni chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi ‘fiber’.

Inaelezwa kuwa matumizi ya juisi ya mbegu za komamanga husaida sana kutoa ahueni kwa wale wenye matatizo ya saratani. Huku ikisaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenda vizuri katika mishipa ya damu, jambo ambalo husaidia presha ya damu na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi.

Mbali na hayo pia husaida sana kulinda meno na kuzuia kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu na maambukizi ya virusi ndani ya mwili, halikadhalika husaidia kutibu madhaifu ya tumbo kama kuharisha na kutopata choo.

Hayo ndiyo machahche ambayo nimeona nishare na wewe mdau wngu leo pengine yanaweza kukusaidia katika kujenga afya yako.

Ndugu yangu kama unateseka na magonjwa mbalimbali ni vyema ufanye utaratibu wa kuwahi kufika Mandai Herbalist Clinic sasa ili upate suluhisho la matatizo yako ya kiafya. Wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment