Wednesday, 24 June 2015

RAIS WA WANAFUNZI WAKITANZANIA KATIKA CHUO CHA MAKERERE ATEMBELEA MANDAI HERBALIST CLINIC ASEMA MAMBO MAZITO KUHUSU TIBA ASILIA


Dk Abdallah Mandai (kulia) akisalimiana na Rais wa Wanafunzi Wakitanzania wa Chuo cha Makerere, Salehe Raphael Kiangu aliyetembelea Mandai Herbalist Clinic.
Leo June 24, 2015, Mandai Herbalist Clinic ilitembelewa na Salehe Raphael Kiangu ambaye ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo Kampala nchini Uganda.

Kwanza ni vyema ikafahamika kuwa Chuo Kikuu cha Makerere ni miongoni mwa vyuo vikuu chuo vikubwa duniani, ambacho pia kimetoa baadhi ya viongozi wengi mashughuli hapa nchini akiwemo hayati Baba wa Taifa Mwal: Julius Kambarage Nyerere na Rais wa awamu ya tatu Mh; Benjamin Wiliam Mkapa, sambamba na baadhi ya mawaziri ambao sitaweza kuwataja kwasasa.
Dk. Abdallah Mandai (kushoto) akiwa ofisni kwake akizungumza na Rais wa Wanafunzi Wakitanzania wa Chuo cha Makerere, Salehe Raphael Kiangu
Mwanafunzi huyo Salehe, mbali ya kuwa mwanafunzi chuoni hapo lakini pia alikuwa ni Rais wa wanafunzi watanzania ndani ya kipindi cha mwaka 2014 hadi 2015.

Rais wa Wanafunzi Wakitanzania wa Chuo cha Makerere, Salehe Raphael Kiangu akiandika katika kitabu cha wageni ndani ya chumba cha kitengo cha habari Mandai Herbalist Clinic

Salehe anasema kuwa yeye kama kijana amekuwa akiamini sana tiba asilia na hushangazwa na vijana ambao wanazibeza tiba asilia.

Hayo ni macheche kati ya yale mengi aliyozungumza katika mahojiano maalum na kitengo cha habari cha Mandai Herbalist Clinic, lakini mahojiano yote unaweza kuyasikiliza hapa chini, ambapo utasikia akizungumzia hali ya tiba asili ilivyo Uganda, pia ataeleza namna alivyoifahamu Mandai Herbalist Clinic na ameleza kuhusu elimu inayotolewa pale Chuoni Makerere  pamoja na kutoa ushauri kwa vijana kuhusu tiba asili.

Bonyeza 'Play' hapo chini ili kusikiliza mahojiano hayo vizuri zaidi

1 comment: