Monday, 22 June 2015

SERIKALI YA AFGHANISTAN IMESEMA KUWA IMEFANIKIWA KUSITISHA SHAMBULIO LILILO LENGA KATIKA BUNGE


Asubuhi tuliripoti taarifa kuhusu kulipuka kwa milipuko mikubwa karibu na bunge la Afghanistani.

Sasa taarifa zinazoendelea kwa sasa ni kwamba serikali ya Afghanistan imesema kuwa imefanikiwa kusitisha shambulio katika bunge na kuweza kuwaua washambuliaji wote.

Hata hivyo, kundi la wapiganaji wa Taleban limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo lilianza na kulipuka kwa gari lililotegwa vilipuzi nje ya bunge kabla ya ufyatuzi wa roketi na risasi.

Pamoja na hayo inaelezwa kuwa wapiganaji hao walishindwa kuingia ndani ya jengo la bunge. Huku Msemaji wa Wizara ya Ndani akisema kuwa hakuna mbunge aliyejeruhiwa, lakini zaidi ya watu 20 walijeruhiwa na vigae vya chupa.

Afisa mmoja wa wizara ya afya amesema kuwa mmoja ya waliojeruhiwa alikuwa katika hali mbaya.

Shambulizi hilo limefanyika wakati bunge lilipokutana ili kumchagua waziri mpya wa ulinzi.

 Endelea kuwa karibu na tovuti hii kwa ajili ya kufikiwa na taarifa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment