Tuesday, 30 June 2015

SERIKALI YATOA ONYO KWA WALE WENYE DHAMIRA YA KUGOMA KUUZA MAFUTA


Miongoni mwa vituo vinavyouza mafuta jijini Dar es Salaam
Kufuatia kuwepo kwa uvumi wa kuwepo kwa mgomo wa wauzaji wa mfuta ya Petrol na Dizel nchini Tanzania

Kufuatia hali hiyo Serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akizungumza Bungeni mijini Dodoma, amesema kwamba serikali itawachukulia hatua wamiliki wa makampuni ya mafuta pale watakapo kiuka na kuvunja sheria ikiwemo kufanya mgomo hali ya kuwa mafuta yapo.

Aidha, Mwijage amesema kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini anawahakikisha wananchi kwamba haiwezi kutokea mgomo wa mafuta nchini, kwa sababu wanajua kwa takwimu katika hifadhi za Dar es Salaam zinaonesha kuwa kuna mafuta ya kutosha.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage
Pamoja na hayo, amesisitiza kuwa sheria na kanuni zinampa mamlaka Waziri kuruhusu mafuta yauzwe, pia sheria za EWURA zinaweza kumfungia mtu yeyote mwenye mafuta anayekataa kuyauza

Mbali na hayo, naibu waziri amewataka wenye vituo kuruhusu mafuta yauzwe na kusisitiza kuwa asitokee mtu yeyote kufanya uvumi huo kuwa ukweli.

Shukrani kwa kuendela kuungana nasi mdau wetu, pia tunapenda kukukaribisha kutangaza biashara yako kupitia website hii, gharama zetu ni nafuu sana. Tupigie simu namba 0716 300 200, 0754 391 743, 0784 300 300. Barua pepe, dkmandaitz@gmail. Au fika ofisini kwetu Ukonga, Mongolandege jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment