Monday, 1 June 2015

SIKU ZOTE TUNASIKIA KUWA UVUTAJI WA SIGARA NI HATARI KWA AFYA, SASA HUKO NCHINI CHINA WAO WAMEAMUA HIVI....!


Uvutaji wa sigara umekuwa na madhara makubwa kwa watumiaji pamoja na watu wa karibu na wanaotumia.

Moja ya madhara ambayo huweza kupatikana kutokana na uvutaji wa sigara ni pamoja na kupata saratani hasa ile ya mapafu.

Kutokana na kutambua madhara hayo Serikali ya China, imeamua kupiga marufuku kuvuta sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing.

Kufuatia agizo hilo maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya wazi na watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa faini.

Inaelezwa kuwa, nchini China kuna wavuta wa sigara milioni mia tatu idadi hiyo ni ya wakati sheria ya kusitisha wavutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa kutekelezeka.

Hata hivyo, watu wengi wanadhani sheria hiyo ya kukataza kabisa uvutaji sigara haitafanya kazi.

Asante kwa kuendelea kuichagua tovuti yetu kama sehemu ya kujipatia habari mbalimbali. tambua tunathamini sana uwepo wako msomaji wetu

1 comment:

  1. makala nzuri lakini serikali haitaki muelimishe mpaka mpate vibali, kazi kwelikweli

    ReplyDelete