Monday, 15 June 2015

TAARIFA KUHUSU MSIBA WA MUFTI SHEIKH ISSA SHAABAN BIN SIMBA PAMOJA NA RATIBA NZIMA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU IPO HAPA


Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Waislamu Tanzania, Mufti Issa Bin Shaaban Simba
Moja ya taarifa ambayo imeripotiwa zaidi leo kupitia vyombo vya habari mbalimbali hapa nchini  pamoja na mitandao ya kijamii ni kuhusu kufariki kwa aliyekuwa Sheikh Mkuu Tanzania, Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba.

Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum amethibitisha kutokea kwa msiba huo pamoja na kutangaza ratiba ya kuaga mwili wa marehemu.

Akitangaza ratiba ya kuaga mwili wa marehemu, Sheikh Salum amesema kuwa “kesho majira ya saa nne asubuhi waislam na Viongozi wote wa kitaifa watajumuika hapa BAKWATA makao makuu Kinondoni Muslim kutakuwa na shughuli za kuuaga mwili wa sheikh pamoja na kumuombea dua na majira ya mchana mwili wa sheikh utasafirishwa kwenda Shinyanga na kule atazikwa siku ya Alhamisi."

Aidha, Sheikh Salum amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika kumuaga Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba.

"Waislamu wa mkoa wa Dar es Salaam na wale wa mikoa ya jirani wanatakiwa kesho saa nne asubuhi kumiminika katika viwanja vya BAKWATA makao makuu ambapo shughuli zote zitafanyika kabla ya kusafirishwa kwa mwili wa marehemu. "

Sheikh Salum akimzungumzia , Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba, amesema kuwa " alikuwa na sifa ya kuwa kiongozi wa waislam alikuwa ni mvumilivu sana na alikabiliwa na changamoto mbalimbali, lakini bado alikuwa ni mvumilivu na msamehevu sana katika utawala wake, ambao umewafanya waislam hadi leo kuwa na utulivu katika nchi yao ni kwasababu ya subira na uvumilivu wake. Kwahiyo tunamtazama na kumjua kwa hilo mheshimiwa Mufti na namna gani alivyoweza kuwaongoza waislam hadi sasa."

Uongozi wa Mandai Herbalist Clinic unapenda kutoa pole nyingi kwa msiba huu wa Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba.

Innaa Lillahi wa inna ilayhi rrajiuun. Sisi wote ni wa mwenyezi Mungu hakika kwake tutarejea mbele yake nyumba yetu.
 

No comments:

Post a Comment