Thursday, 18 June 2015

TABIBU MANDAI AKIELEZEA NAMNA YA KUKABILIANA NA VIDONNDA VYA TUMBO KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI(AUDIO)

Habari za leo mdau wetu wa www.dkmandai.com najua leo ndugu zetu waislam wameanza rasmi mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Kuna baadhi ya watu huhitaji kufunga katika mwezi huu ili kujipatia swawabu na hata afya pia, lakini hujikuta wakishindwa kufanya hivyo kutokana na tatizo la vidonda vya tumbo.

Leo Tabibu Mandai ameamua kukwambia namna ya kukabiliana na tatizo hilo ili uweze kufunga na kutimiza nguzo hii ya nne ya kiislamu.

Karibu hapa chini umsikilize Tabibu Mandai akielezea namna ya kukabiliana na vidonda vya tumbo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani


Swaum ni yenye faida za kiafya, huchukuliwa kimsingi kuwa ni namna ya kuisafisha nafsi kiroho. Kwa mmojawapo kujizuia dhidi ya starehe za kidunia, japo kwa muda mfupi, mfungaji hupata huruma ya kweli kwa wanaopatwa na njaa, kadhalika na kuongezeka kwa maisha yake ya kiroho.

No comments:

Post a Comment